Watu wawili wamefariki dunia papo hapo
na wengine kumi na mmoja kujeruhiwa vibaya wakati wakifanya kibarua cha
kushusha nguzo za kusambazia nishati ya umeme vijijini kupitia kampuni
ya moja ya Derm katika kijijini cha Bisumwa wilayani Butiama mkoani
Mara.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamesema tukio
hilo limeokea leo saa 3.30 asubuhi katika kijiji cha Bisumwa wilayani
Butiama,ambapo vibarua hao kutoka kijiji cha sabasaba baada ya kufika
kijijini hapo na lori hilo aina ya Scania yenye namba za usajili T 787
CUL wakiwa juu ya sheena hiyo ya nguzo na wakati wajaribu kufungua
mikanda kwa ajili ya kuzishusha nguzo hizo zilishuka kwa kasi kubwa
sambamba na wao hatua ambayo imesababisha watu wawili kufariki dunia kwa
kugongwa na nguzo hizo huku wengine wakipata majeraha makubwa yakiwemo
ya kuvunjika kwa miguu.
Viongozi wa halmashauri ya Butiama wakiongozwa na
mwenyekiti wake Bw Magina Magesa, ambao walifika muda mfupi baada ya
tukio hilo kutokea kwa ajili ya kutoa msaada kwa majeruhi hao,pamoja na
kutoa pole lakini wametaka kampuni zinazohusika kusambaza nishati ya
umeme katika vijiji vya mkoa wa Mara kuchukua tahadhari wakati wa
kusafirisha nguzo hizo ili kuepuka ajali mbaya kama hiyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa polisi mkoa wa Mara
kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Paul Kasabago, akizungumza na ITV
kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja
marehemu kuwa ni Masui Magibo (20) na Salabanze John (22) wote wakazi wa
kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama na kwamba majeruhi wote wamelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Mara mjini Musoma kwa ajili ya matibabu
zaidi.
0 comments:
Post a Comment