Khloe Kardashian na The game walijiachia pamoja kwenye night club
kiasi cha kuwapa watu mashaka kwamba wawili hao wapo kwenye uhusiano wa
kimapenzi hivi sasa.
Khloe alikuwa wa kwanza kukanusha uhusiano huo na kusema kwamba walikuwa wapo kwenye starehe kama marafiki.
Hivi karibuni The game amepata nafasi ya kuzungumzia kuhusu kile kilichotokea na ametoa exclusive mpya.
Akiwa kwenye radio ya BBC Radio1 Extra The game alisema asingeweza
kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Khloe kwasababu alikuwa na uhusiano na
dada yake Kim kipindi kilichopita.
“Watu hawajui kuhusu mimi na Khloe kwamba tumejuana miaka 12
iliyopita. Nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kim Kardashian kwa muda
kidogo sana. Kanye West alikuwa bado mshkaji kipindi kile na hadi sasa
bado ni mshkaji wangu na najua Kim anakaribia kuwa mke wake na tayari
wanafamilia. Khloe pia ni mshkaji na tuko poa pamoja kwa hiyo hizo
tetesi kati yangu na Khloe hazina ukweli”
CREDIT: AYO
0 comments:
Post a Comment