Husein machozi ndiye msanii mwingine mkongwe aliyetokea kufunguka juu
ya msanii Diamond Platnumz,wamewahi kufunguka wasanii wengi ,ikiwemo
msanii mkongwe maarufu Alikiba ,na msanii mwingine mchanga Dayna Nyange
kwa madai kuwa Diamond alimuibia Beat yake nakuitumia kwenye track yake
ya MyNumberOne, Husein Machozi amefunguka nakuweka wazi kuwa hamkubali
Diamond,na nyimbo karibia zote alizowahi ku-hit nazo ni zaku-copy na
kupaste ,kutoka kwa wasanii wengine hasa wachanga ambao hawana sauti
katika media, kutokana nayeye ameshajipatia umaarufu teyari,nakuzidi
kukubalika na watu wa kila sector hasa kwenye media.
Hussein Machozi |
Beef ya Husein na Daimond ilianza kipindi hicho wakati Diamond yupo bado katika harakati za kutafuta umaarufu na kushikilia level za juu,Diamond aliiba wimbo wake ulioitwa Haikai,nakuichukua kuibadilisha jina na kuiita kizaizai,moja ya nyimbo ambayo ilimpa umaarufu Diamond,nakumsaidia kumweka katika chart za juu kimuziki, “I am still one of the best artistes in the region, and that is why artistes such as Diamond had to sample my song and call it Kizaizai to become famous. I have actually recorded many songs that I will release soon; he should copy those, too”alisema Husein machozi akiwa anahojiwa na moja ya media ya huko nchini Kenya.
Ally Kiba na Dayna Nyange |
Husein alikiri kuwa , tatizo la wasanii wa siku hizi kama Diamond,ni kuiga mafanikio ya wasanii wakubwa wanchi za wengine,na kutaka kuibuka tu ghafla,kutaka kuishi kifahari kama wao,bila kujua kuwa imewachukua miaka mingapi yakuhangaika katika game hadi kufikia hapo walipo.Alialisema tatizo la diamond ni kutaka kushikilia kwenye level ambazo haziwezi,na ndio maana karibia nyimbo zake zote amezikopi kutoka kwa wasanii wenzake wa Bongo fleva, ikiwemo Ngololo na Nataka Kulewa.
0 comments:
Post a Comment