KhAA! Mshiriki wa Shindano la Miss Kiswahili mwaka 2009 ambaye kwa
sasa yuko nchini China akijitafutia maisha, Rehema Fabian amenaswa laivu
akiwa kimahaba na kibabu cha kizungu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mnyetishaji wetu
ambaye naye yuko nchini humo alisema kuwa kwa sasa mrembo huyo
anajiachia na babu huyo ambaye kwa kumwangalia harakaharaka anaweza kuwa
sawa na mjukuu wake.
“Unajua mapenzi ya wazee ni mazuri sana, kwanza wanajua kubembeleza,
isitoshe hawakupi msongo wa mawazo mara kwa mara kama yalivyo mapenzi ya
vijana na ndiyo maana Rehema akaona bora ajiachie na kibabu,” alisema
mtonyaji huyo.
Baada ya kupata ‘infomesheni’ hizo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta
Rehema ili kujiridhisha kuhusiana na stori hiyo ambapo kwa upande wake
alianza kucheka kisha kudai aachwe ale ujana.
“Ahaha! Mshaanza mambo yenu, niacheni jamani nile ujana,” alisema Rehema.
“Ahaha! Mshaanza mambo yenu, niacheni jamani nile ujana,” alisema Rehema.
0 comments:
Post a Comment