Chris Brown baada ya kuvunja sheria za rehab alifukuzwa na baadae kukamatwa, hivi sasa amewekwa jela kwa muda wa mwezi mmoja.
Mtandao mmoja wa huko Marekani umeripoti kwamba Chris Brown yupo
kwenye hali mbaya ndani ya gereza hilo kiasi kwamba hali chakula,usiku
halali,anaongea peke yake na maisha ya humo ndani ni magumu kwake.
Wanaendelea kuripoti kwamba Chris anakunywa maji tu na wakati
mwingine anapewa juisi ya machungwa.Huwa anapewa sandwich kwenye chombo
kibovu na Chris Brown huwa anakataa hiyo sandwich.
Chris bado anakabiliwa na mashtaka mengine ambayo ni kumpiga kijana
mmoja na kama kesi hiyo ikimuendea vibaya anaweza kwenda jela miaka 4.
Taarifa zinazotoka hivi sasa ni kwamba mwanasheria wa Chris Brown
anafanya juhudi zote za kumlipa kijana huyo ili mteja wake akimaliza
mwezi mmoja wa jela asiwe na kesi yoyote.
Mwezi huu mmoja anaotumikia Chris ni kutokana na jaji kumtaka akae
rehab baada ya kuvunja sheria alizowekewa baada ya kesi ya Rihanna.
Lakini pia akavunja sheria za Rehab na kujikuta anafungwa kwa mwezi
mmoja.
0 comments:
Post a Comment