Kama unakumbuka shindano la kumtafuta mtu mwenye sura mbaya kupita
wote nchini Tanzania liliwahi kutokea na mshindi akaibuka jamaa mmoja
anaitwa Masudi. Miongoni mwa watu ninaowakumbuka kushiriki shindano lile
ni pamoja na Marehemu Remmy Ongala na Mzee Jangala ambaye enzi zile
alikuwa muigizaji maarufu sana hususani katika vipindi vya radioni.
Nakumbuka katika mchezo mmoja ambao ulinivutia na kuufuatilia sana
alikuwa na mwanae wa kiume anayeitwa Mshamu.
Bahati mbaya shindano lile halijawahi kurudiwa tena. Masudi, ambaye
baada ya kuibuka mshindi alidai anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa
“wachumba” wanaotaka awaoe, anabakia kuwa mtu mwenye sura mbaya kupita
wote nchini Tanzania…kama kweli.
Hivi karibuni, nchini Zimbabwe, pengine kwa kufuata mfano ule wa
Tanzania, nao wamekuwa na shindano la kumtafuta mwanaume mwenye sura
mbaya kupita wote nchini humo.
Mshindi, kwa mwaka wa pili mfululizo, ameibuka kuwa William Masvinu
unayemuona hapo pichani juu. Mbali ya kupewa zawadi ya mtoto wake mmoja
kulipiwa ada ya shule, William pia alichukua dola za kimarekani $100.
Tofauti na Masudi wetu, William tayari ana mke, Alice Chabhanga. William
anasema mkewe ndio mwanamke pekee aliyemkubali na kwa sababu hiyo ana
uhakika kwamba hana mshindani.
Alaa..hata “ubaya” una faida yake…
0 comments:
Post a Comment