Friday, July 11, 2014
- 9:14 AM
- Unknown
- MAJANGA, SOCIAL
- No comments
Hii imeripotiwa kutoka katika mtandao mmoja huko Nigeria Kuwa Mwanaume huyu Shoga amejipatia Mtoto wa kiume akiwa amezalishwa na mwanume mwenzake!!! soma maelezo haya chinni
This is the emotional moment as gayy dads gives birth and met their son for the first time..The couple’s emotional moment was captured by photographer Lindsay Foster who wrote
“I had the opportunity to photograph this amazing birth on June 27 for a surrogate and two expecting and anxious daddies. Hours were spent with them in the hospital room while the surrogate mom was laboring and I got to know them quite well.They are two compassionate people who felt all the emotions that every new parent feels. They asked all appropriate questions of the birthing mom and the midwife and educated themselves as best as they could for their son’s arrival. I am so proud of these two dads.”
- 9:00 AM
- Unknown
- MAJANGA, SOCIAL
- No comments
Mzungu mmoja huko majuu aliamua kujibandika ngozi nyeusi ili aonekane kama mtu mweusi..kwa
kuwa wadada wengi wanazimika na wanaume weusi kuliko weupe. Dah! hili kweli badaa!!!
- 8:44 AM
- Unknown
- 18+, MAJANGA, SOCIAL
- No comments
Utandawazi umeendelea kuwaangamiza kaka zetu wanaopenda kuiga mambo ambayo hayana mashiko katika jamii yetu hasa ya kitanzania....
Katika upaparazi wetu, mtandao huu umefanikiwa video ya shoga huyu akiwa anapata kitu roho inapenda maeneo ya sinza jijini dar es salaam!!!
- 8:34 AM
- Unknown
- MAJANGA, SOCIAL
- No comments
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.
MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa miaka, 32 umeokotwa jana na kufanya idadi ya wanawake waliouawa mpaka sasa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kufikia nane.
Wanawake hao nane waliouawa kikatili mpaka sasa wana umri kati ya miaka 18-32.
Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.
Katika kuonyesha kuwa wamekerwa na vitendo hivyo, baadhi ya wananchi wilayani humo, walizingira Kituo Kikuu cha Polisi Nachingwea, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne wakitaka polisi kuwaruhusu kuwa waue watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, amesema wananchi hao wenye hasira walikuwa wamezunguka kituo hicho cha polisi wakitaka kuwaua watuhumiwa watatu wanaoshukiwa kuwa ndio wahusika wa baadhi ya mauaji ya wanawake hao.
- 5:28 AM
- Unknown
- MAJANGA, SOCIAL
- No comments
PICHA: WANAWAKE 20 WATOA USHUHUDA JUU YA KUFANYA MAPENZI NA WAGANGA WA KIENYEJI ILI KUPATA UJAUZITO.
Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito baada ya kukaa muda mrefu bila watoto, wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.
Kamanda Kiondo akielezea kuhusu uhalifu wa Sangoma walionaswa kwa kufanya ngono na wake wa vigogo.
Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake hao umebaini kuwa, waume wao wanafanya kazi katika nyadhifa za juu serikalini, wengine ni wastaafu na kwamba waume hao hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
...Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.
Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA
Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani ‘kufuli’ za wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa na polisi kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.
Baadhi ya watuhumiwa wa sakata hilo.
KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?
“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.
Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema ni kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi 10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Kamanda Kiondo akionesha baadhi ya nguo za ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa ngono na sangoma hao.
Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC
Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.
Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.
Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya waandishi wa habari.
“Ninaamini kuwa kwa vitendo hivyo vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema Kamanda Kiondo.
...Tunguli zikiteketezwa kwa moto.
Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.
- 3:08 AM
- Unknown
- SIASA
- No comments
Ifuatayo ni kauli ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bumbuli Tanga kuhusu Naibu waziri ambae pia ni mbunge wa Bumbuli January Makamba.
Amenukuliwa akisema >>> ‘January anafanya kazi nzuri ya ubunge pia ananisaidia sana kwa kazi ya wizara niliyompa, unajua January alipogombea Ubunge alinificha nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini, baadae alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa’
‘Nikamtakia heri… kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli, nimesikia anafikiria mambo makubwa… hajaniambia mi nimesikia tu, namtakia kila la heri…. haya mambo anaamua Mungu wala hayalazimishwi’
‘Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki, Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa, mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani, kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea, mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake…. 2005 ikawa wakati wake nikapata, na wewe usipopata sasa usiweke nongwa” – JK
- 2:55 AM
- Unknown
- CELEBRITIES, SOCIAL
- No comments
Staa wa muziki wa kizazi Kipya Bongo,Nasib Abdul 'Diamond', usiku wa kuamkia leo aliwasili nchini akitokea Marekani ambako alienda kwa ajili ya kushiriki kwenye tuzo za BET ,zilizomalizika hivi karibuni, alitua kwenye Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kupokelewa na umati wa mashabiki kibao majira ya saa 5 usiku.
Diamond akiwanyooshea mikono baadhi ya watu waliyojitokeza kumpokea mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Julius Nyerere,usiku wa kuamkia leo.
Wema Sepetu wa pili kutoka kushoto,akifurahia jambo na mashoga zake kwenye Uwanja wa Julius Nyerere wakati alipoenda kumpokea mpenzi wake huyo.
Baadhi ya mashabiki wa Diamond wakiwa wamenyanyua mabango tayari kwa kumpokea msanii huyo.
Watu mbalimbali wakichukua baadhi ya matukio ya kuwasili kwa Diamond kwa kupiga picha.
Diamond (kulia), akisalimiana na mama yake mzazi Bi,Sanura, mara baada ya kutua nchini.
Wema Sepetu, akiwa amekumbatiana na Diamond mara baada ya kufika nyumbani kwao na msanii huyo.
Diamond,Wema wakicheza wimbo wa mdogomdogo,muda mfupi baada ya kutelemka kwenye gari wakitokea uwanja wa ndege.
Diamond akiwa katika pozi na jamaa zake baaada ya kuwasili nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo.
Muziki ulizidi kukolea kwa mashabiki, Wema na Diamond.
Baadhi ya mashabiki wa Diamond wakicheza staili ya Kiduku kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar ,wakati wa kumpokea Diamond.
(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
Subscribe to:
Posts (Atom)