Friday, July 11, 2014

Staa wa muziki wa kizazi Kipya Bongo,Nasib Abdul 'Diamond', usiku wa kuamkia leo aliwasili nchini akitokea Marekani ambako alienda kwa ajili ya kushiriki kwenye tuzo za BET ,zilizomalizika hivi karibuni, alitua kwenye Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kupokelewa na umati wa mashabiki kibao majira ya saa 5 usiku.

Diamond akiwanyooshea mikono baadhi ya watu waliyojitokeza kumpokea mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Julius Nyerere,usiku wa kuamkia leo.

Wema Sepetu wa pili kutoka kushoto,akifurahia jambo na mashoga zake kwenye Uwanja wa Julius Nyerere wakati alipoenda kumpokea mpenzi wake huyo.

Baadhi ya mashabiki wa Diamond wakiwa wamenyanyua mabango tayari kwa kumpokea msanii huyo.

Watu mbalimbali wakichukua baadhi ya matukio ya kuwasili kwa Diamond kwa kupiga picha.

Diamond (kulia), akisalimiana na mama yake mzazi Bi,Sanura, mara baada ya kutua nchini.

Wema Sepetu, akiwa amekumbatiana na Diamond mara baada ya kufika nyumbani kwao na msanii huyo.

Diamond,Wema wakicheza wimbo wa mdogomdogo,muda mfupi baada ya kutelemka kwenye gari wakitokea uwanja wa ndege.

Diamond akiwa katika pozi na jamaa zake baaada ya kuwasili nyumbani kwao Sinza Mori jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo.

Muziki ulizidi kukolea kwa mashabiki, Wema na Diamond.

Baadhi ya mashabiki wa Diamond wakicheza staili ya Kiduku kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar ,wakati wa kumpokea Diamond.

(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)

0 comments:

Post a Comment

Click here

Click here

Popular Posts