 
 Jide akiwa na jumewe Gardner.
UNAWEZA ukakataa lakini ndivyo ilivyotokea, ndoa ya mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel  Fikirini Habash ‘Kapteini’ na Mbongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’  iliyofungwa miaka 9 iliyopita inadaiwa kuingia kidudu kufuatia mke huyo  kuomba aandikiwe talaka, ni Ijumaa Wikienda pekee lenye uthubutu wa  kuripoti mkasa wote.Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Jide au  Lady Jaydee alifikia uamuzi huo baada ya Gardner kupata kazi ya  kutangazia redio moja nchini Kenya.
HABARI KAMILI
 
Mnyetishaji wa kisanga hiki, aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa marabaada ya mume huyo kupata mchongo mzima alirudi nyumbani akiwa na furaha na kumwambia mkewe kuhusu bahati hiyo.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Baada ya Gardner kupata mchongo wote wa kazi alikwenda mbio nyumbani kwake Kimara (Dar) ili akamwambie mkewe.
“Pia katika safari ya  kwenda Kenya kupiga mzigo ilikuwa aende na mkewe huyo kwa sababu  lilikuwa suala la kuhamisha makazi yao Tanzania,” kilisema chanzo hicho.
 
 Jide na Gardner siku ya ndoa yao.
JIDE AHAMAKI
 
Chanzo kikatoboa kwamba Gardner alipofika nyumbani kwake na kumweleza mkewe, alikumbana na kitu ambacho hakukitarajia.
“Komando (Jide) alihamaki na kumjia juu akisema yeye hawezi kuondoka Tanzania kwenda  kuishi Kenya, kama Gardner analiona jambo hilo ni heri kwake,  amuandikie talaka yake na kuachana ili kila mmoja achukue hamsini zake,”  chanzo kilizidi kuporomosha maneno.
KWA NINI JIDE HAKUPENDA?
 
Habari  zilizidi kuanikwa kwamba Jide au Binti Machozi alifikia uamuzi huo  baada ya kugundua kuwa kitendo cha kwenda kuishi Kenya kitaua bendi yake  ya Machozi na sehemu ya biashara ya NyumbaniLounge iliyopo Ada-Estate, Kinondoni, Dar.
MBAYA ZAIDI
 
Taarifa  zikazidi kumiminika kwamba, mbali na Jide au Anakonda kuhofia biashara  zake kufa, lakini pia hakupenda Gardner aondoke hata peke yake kwa  sababu yeye ndiye meneja wa miradi hiyo miwili.
“Mimi nilipopata habari hizo nilikutana  na Jide nikamuuliza, akanijibu ameamua iwe hivyo tu, kikubwa mumewe  (Gardner) aamue moja kati ya hayo mawili kwani yeye ana haki akiwa kama  mkewe wa ndoa,” kilisema chanzo kikimkariri Jide.
GARDNER AISHIWA NGUVU
 
Kufuatia majibu ya mkewe, taarifa zinasema mtangazaji huyo ambaye alishawahi kupiga mzigo kwenye kituo cha Radio Clouds FM cha jijini Dar alijikuta akiishiwa nguvu na kuachana na dili hilo mara moja.
“Gardner alisalimu amri kwa mkewe,  akaamua kuachana na dili la kwenda kutangaza Kenya. Lakini alifikiri  sana akasema ni kweli kuhamia Kenya kungeua miradi yao ya Tanzania maana  ingekosa msimamizi wa kuaminika,” chanzo kiliweka wazi.
KAMA ANGEKWENDA KENYA
 
Siri  hiyo iliyovujia mikononi mwa Ijumaa Wikienda haikuishia hapo, ilizidi  kuanikwa kwamba kama Kapteini angekwenda Kenya na kuanza kazi, ilikuwa  alipwe mshahara wa shilingi za Kenya laki 3 kwa mwezi (kama milioni 6 za  Tanzania).
NAFASI YAKE BADO IPO
 
NAFASI YAKE BADO IPO
Mpashaji wetu alisema kwamba  nafasi ya Gardner kwenye kituo hicho cha redio ambacho hakikutajwa, bado  ipo lakini tamko la Jide nalo li hai, kwa vile hakubatilisha, endapo  mumewe atataka kwenda hata kesho (Jumanne) aandike 
 talaka.
WIKIENDA NA GARDNER
 
Baada  ya kunyetishiwa taarifa nzima, juzi gazeti hili lilimsaka Gardner. Kwa  njia ya simu lilimkosa, likamfuata Nyumbani Lounge. Lilipomkuta  lilimsimulia kisanga chote cha ndoa yake kutikiswa na kitendo cha yeye  kupata kazi Kenya ambapo alijibu hivi:
“Ndoa ni nzuri, ni kweli ilikuwa niende  Kenya, nilipata kazi kule lakini kama familia ilikuwa lazima tukae na  kupanga, mwenzangu hakuafiki.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”
Wikienda: “Ni kweli shemeji ameomba uchague mawili, umwandikike talaka au uende Kenya?”
Gardner: “Ndiyo maana nimesema ndoa nzuri, lazima makubaliano yawepo, mke anaweza kuonesha msimamo wake na mume kama utakaa chini na kuufikiria ukapata jibu unakubaliana na mke wako wala hakuna ubaya.”
Wikienda: “Kule mshahara wako ungekuwa shilingi ngapi?”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”
Gardner: “Hiyo sasa ni siri ya makubaliano.”
Wikienda: “Kwa nini usiamue kwenda tu?”
Gardner: “Nimekwambia ndoa nzuri.”
JIDE BIZE
Juhudi za kumpata Jide ziligonga mwamba baada ya muda wote kuwa bize na shoo ya kukata na shoka aliyokuwa akiifanya siku hiyo kwenye ukumbi huo akikimbiza na nyimbo zake kali za zamani na hizi mbili zilizogeuka nyimbo za taifa, Joto Hasira na Yahaya.
RAFIKI WA GADNER AMCHAMBUA JIDE
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
Rafiki wa karibu na Gardner (jina tunalo) ambaye alisikia mahojiano ya mtangazaji huyo na Ijumaa Wikienda, alisubiri jamaa aondoke ambapo alianza kumchambua Jide.
“Nataka kuwaambia kitu, Jide ni mwanamke jasiri sana. Ana msimamo na anaposhikilia msimamo wake hatengui hasa kama atabaini kuwa yupo sahihi.
“Ni kweli jamaa (Gardner) alipata kazi  Kenya tena mshahara mzuri tu, lakini mama (Jide) akaweka ngumu hakuna  kwenda,” alisema rafiki huyo.
-GPL






 12:26 AM
12:26 AM

 
 
 
 
 

0 comments:
Post a Comment