Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu. |
MMOJA wa wajomba wa Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu, Jacob Temu
amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumtishia maisha mlimbwende huyo.
Tukio la kukamatwa kwa Jacob lilikuja baada ya kutishia kumuua kwa
maneno Hoyce pamoja na shangazi yake ambaye ni Hilda Temu, katika
mabishano ya wanaukoo juu ya sehemu ya kumzika ndugu yao, marehemu
Emmanuel Nambuo Temu (33).
Hoyce aliliambia gazeti hili kuwa alitishiwa maisha kwa maneno wakati
wa kikao cha wanaukoo kilichofanyika katika viwanja vya baa ya Rose
Garden kujadili ni wapi pa kumzika marehemu Emmanuel, aliyefariki dunia
jijini Dar Februari 16, 2014. Wakati baadhi ya wanafamilia na wosia wa
marehemu wakitaka azikwe walipozikwa bibi na babu yake, Jacob alipinga
hali iliyosababisha Hilda kufungua kesi katika Mahakama ya Wilaya ya
Temeke. Jacob alikamatwa na polisi baada ya kufunguliwa jalada yenye
kumbukumbu na OB/RB/3554/2O14 KUTISHIA KUUA ambapo kesi hiyo iko katika
Kituo cha Polisi cha Oysterbay jijini Dar.
Katika kesi aliyoifungua Hilda na kusikilizwa hukumu kutolewa Jumatano iliyopita, Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Temeke, Kassim Sapi Mkwawa aliamuru mwili wa Emmanuel uzikwe katika shamba la mjomba wa marehemu Dk. Mercezederc Nambuo Temu ambaye ni kiongozi wa ukoo katika Kijiji cha Kitahie, mkoani Kilimanjaro. Awali kesi hiyo ya madai namba saba ya mwaka 2014, ilifunguliwa mahakamani hapo na Hilda Lewi Nambuo Temu, ambaye ni mama mzazi wa marehemu, akitaka mazishi ya mwanaye Emmanuel yafanyike Kijiji cha Kitahie Old Moshi mkoani Kilimanjaro lakini Jacob alipinga. Hakimu Mkwawa wakati wa kutoa hukumu hiyo alisema:

“Baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili nimebaini kuwa pande
zote mbili za ndugu wanachobishana si Kijiji cha Kitarara wala Kitahie
bali hawataki marehemu azikwe kwenye shamba la ukoo. “Lakini kwa kuwa
baba mkubwa wa marehemu Dk Mercezederc amekubali marehemu Emmanuel
azikwe kando ya shamba lake lililopo Kitahie, hakuna aliyepoteza baina
ya pande zote mbili, hivyo marehemu akazikwe hapo,” alisema hakimu na
akasema gharama za kesi kila upande ujibebee. Kutokana na h
0 comments:
Post a Comment