Hapa duniani kwasasa kuna mabilionea 1645 , kutokana na takwimu
zilizotolewa na Forbes. Kwa mwaka jana bara la Afrika lilikua na
mabilionea 20 lakini kwa mwaka huu wameongezeka mabilionea 9 na mmoja
wapo ni mtanzania. Kwa upande wa sanaa ya hapa Bongo basi tunaweza
kusema Diamond na Lady jaydee ndio wanaongoza kwa mkwanja labda ni
kwasababu ya uwekezaji wao wanaofanya na kila kukisha kutuonesha mapesa
na magari wanaomiliki lakini sio mbaya ukamjua tajiri namba moja
Tanzania na namba mbili kwa Afrika mashariki akiachwa na Sudhir
Ruparelia kutoka Uganda mwenye utajiri wa bilioni 1.1 za kimarekani .
Anaitwa Rostam Aziz, 53 ndio bilionea pekee Tanzania. Anamiliki
asilimia 35 ya mtandao wa Vodacom, Mtandao mkubwa zaidi nchini wenye
watumiaji zaidi ya millioni 10.Pia Rostam anamiliki mgodi wa Caspian
Mining.pia anamilikia asilimia fulani kwenye bandari ya Dar-es-salaam.
Na pia anafanya biashara za nyumba nchi za Tanzania, Dubai, Oman and
Lebanon. Rostam ana utajiri wenye thamani ya bilioni 1 za kimarekani.
Ikumbukwe kwamba Akon ndio msanii tajiri kuliko wote Afrika na
utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 80 na kwa mwaka huu ameanza
kampeni ya kuzipa mwanga nyumba zaidi ya milioni moja katika nchi za
afrika magharibi na afrika ya kati.
Tujiulize ni lini wasanii wa kibongo watafika level kama alizofika
Akon na sio kwa kipato bali kwa ile hali ya kurudisha shukrani kwa jamii
na kuacha kuturingishia utajiri wao.
0 comments:
Post a Comment