MKALI wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameibuka na kufungukia ishu iliyozagaa mitandaoni kuwa alikamatwa Marekani.



Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Dimpoz alisema picha
zinazomwonesha akiwa chini ya ulinzi si tukio la kweli bali ni sehemu ya
video ya wimbo wake mpya ambayo alikwenda kurekodia nchini humo.
“Sikuwa nimekamatwa kiukweli, ile ilikuwa ni sehemu tu ya video ya
wimbo wangu ambao nilikuwa narekodi, mashabiki wangu wasinielewe vibaya.
Nipo poa tu,” alisema Dimpoz.
0 comments:
Post a Comment