Poleni vijana.
Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya
ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa
Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda
wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye
operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga
kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM,
kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi
ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua,
kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa
Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”
Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.

0 comments:
Post a Comment