DK CHENI
MINONG’ONO na uvumi unaotambaa kwa kasi kuwa anajihusisha na taasisi ya wajenzi huru (Freemasons), unazidi kumtesa Dk Cheni msanii wa filamu za Kibongo, kwa madai ya kwamba anajisikia vibaya anaponyoshewa vidole na baadhi ya wadau wa tasnia hiyo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mwandishi wetu alisikia fununu kutoka
kwa wadau wengi wa filamu wakiwemo wasanii wenzake wakidai kuwa Dk.
Cheni ni mwanachama halali wa taasisi hiyo ndiyo maana mambo yake ni
mazuri kifedha ukilinganisha na wasanii wengine wanaoaminika kuwa na
uwezo mkubwa wa kuigiza kuliko yeye.
“Kila dalili inaonesha kabisa Dk Cheni ni
Freemason, angalia mavazi yake mengi ni meusi, machata na alama kibao
zinazohusishwa na taasisi hiyo, angali fedha aliyonayo, angalia hata
gari lake lilivyojaa alama za ajabu ajabu, huyu jamaa ni Freemason
kabisa,” alisema mdau mmoja wa filamu ambaye hakutaka jina lake
liandikwe gazetini alipozungumza na mwandishi wetu.
Kauli kama hizo zimekuwa zikitolewa kwa nyakati tofauti na baadhi ya wasanii wenzake.
Dk. Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai hayo alikuwa na haya ya kusema:
Dk. Cheni alipotafutwa kwa njia ya simu Jumapili ya wiki iliyopita na kuulizwa madai hayo alikuwa na haya ya kusema:
Dk Cheni Afunguka
“Dah! na wewe umeyapata kaka? Hakika naumia sana na madai hayo,
yamevuma sana kwa wadau, tena baadhi yao ni watu ninaowaheshimu sana,
jamani mimi siyo Freemason, naigiza, kazi zangu za u-MC zinaniingizia
kipato, najiwekea akiba.
“Si mtu wa starehe, nawekeza katika biashara ndogondogo, madai haya ya Freemason yananitesa sana ila namwachia Mungu,” alisema
0 comments:
Post a Comment