MREMBO mmoja ambaye alihu-dumu kwenye nyumba ya kulala wageni na baa (jina tunalo) iliyopo Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha,
Blandina Michael (33) amekutwa amekufa kwenye moja ya vyumba vya nyumba
hiyo huku chanzo cha tukio hilo kikihusishwa na vitendo vya
ushirikiana.
Taarifa za awali zilimtuhumu mmiliki wa nyumba ya wageni moja ambaye
pia anajihusisha na biashara za madini (jina tunalo) kwamba alimtoa
kafara mhudumu huyo. Ilidaiwa kuwa, kila mwaka mtu mmoja katika biashara
zake hupoteza maisha ghafla.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alipoongea na Uwazi juzikati
alikanusha vikali tuhuma hizo na kueleza kuwa yeye ni muumini mzuri wa
imani yake.
‘’Hao watu wanapotosha sana, unajua kuna mwaka mwanaume mmoja alikufa
ghafla kwenye nyumba yangu ya kulala wageni, alikuja na mpenzi wake ila
alimeza Viagra ambazo hata polisi walizikuta mezani.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
“Sasa watu wasio na nia njema na mimi tukio hilo wanaliunganisha na hili kwamba nawatoa kafara,” alisema.
Undani wa Kifo Chake
Kifo cha Blandina kilitokea ndani ya chumba huku mtu mmoja anayedaiwa
kuwa mpenzi wake aliyejulikana kwa jina moja la Timo, mkazi wa eneo
hilo akihojiwa na polisi.
Mrembo huyo ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Tanga, anaelezwa na bosi
wake huyo kwamba alikuwa kama mtoto wa familia yake kwa vile alimwamini
sana. Alifanya kazi hapo kwa miaka 8 na hakuwa na tatilo la kiafya.
Bosi wa Mrembo Huyo
Bosi huyo alisema mwili wa marehemu uligundulika baada ya mfanyakazi
mwenzake wa kiume kumpigia simu saa 2 asubuhi ambapo simu yake ilikuwa
ikiita bila kupokelewa ndipo alipoamua kwenda kumgongea katika chumba
hicho.
Alisema baada ya kufika alishangaa kukuta mlango wa chumba chake uko wazi na alipochungulia alibaini kwamba Mrembo huyo (Blandina) alikuwa amefariki dunia.
Hata hivyo, polisi baada ya kufika na kuufanyia uchunguzi wa awali
mwili wa Mrembo huyo hawakugundua kuwepo kwa jeraha lolote linaloashiria
kuuawa, ingawa mwili huo ulipelekwa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalam
katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha
limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali hiyo.
Credit: Gpl
0 comments:
Post a Comment