Showing posts with label MAJANGA. Show all posts
Showing posts with label MAJANGA. Show all posts

Friday, July 11, 2014

Hii imeripotiwa kutoka katika mtandao mmoja huko Nigeria Kuwa Mwanaume huyu Shoga amejipatia Mtoto wa kiume  akiwa amezalishwa na mwanume mwenzake!!! soma maelezo haya chinni

This is the emotional moment as gayy dads gives birth and met their son for the first time..The couple’s emotional moment was captured by photographer Lindsay Foster who wrote

“I had the opportunity to photograph this amazing birth on June 27 for a surrogate and two expecting and anxious daddies. Hours were spent with them in the hospital room while the surrogate mom was laboring and I got to know them quite well.They are two compassionate people who felt all the emotions that every new parent feels. They asked all appropriate questions of the birthing mom and the midwife and educated themselves as best as they could for their son’s arrival. I am so proud of these two dads.”


Mzungu mmoja huko majuu aliamua kujibandika ngozi nyeusi ili aonekane kama mtu mweusi..kwa 
kuwa wadada wengi wanazimika na wanaume weusi kuliko weupe. Dah! hili kweli badaa!!!


Utandawazi  umeendelea  kuwaangamiza  kaka  zetu  wanaopenda  kuiga  mambo  ambayo hayana mashiko katika jamii yetu hasa ya kitanzania.... 

Katika  upaparazi  wetu, mtandao  huu  umefanikiwa video ya  shoga  huyu akiwa anapata kitu roho inapenda maeneo ya sinza jijini dar es salaam!!!
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga.

MWILI wa mwanamke mwingine aliyetambulika kwa jina la Zuhura Mtenda mwenye umri wa miaka, 32 umeokotwa jana na kufanya idadi ya wanawake waliouawa mpaka sasa katika Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi kufikia nane.

Wanawake hao nane waliouawa kikatili mpaka sasa wana umri kati ya miaka 18-32.
Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.

Katika kuonyesha kuwa wamekerwa na vitendo hivyo, baadhi ya wananchi wilayani humo, walizingira Kituo Kikuu cha Polisi Nachingwea, kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa nne wakitaka polisi kuwaruhusu kuwa waue watuhumiwa watatu wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ambapo polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Renatha Mzinga, amesema wananchi hao wenye hasira walikuwa wamezunguka kituo hicho cha polisi wakitaka kuwaua watuhumiwa watatu wanaoshukiwa kuwa ndio wahusika wa baadhi ya mauaji ya wanawake hao.
Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa

IMEBAINIKA kuwa miongoni mwa wale wanawake 20 waliodai kufanyishwa ngono na waganga wa kienyeji ‘sangoma’ ili kupata ujauzito  baada ya kukaa  muda  mrefu  bila watoto,  wamo wake wa vigogo Bongo, Uwazi limechimba.

Kamanda Kiondo akielezea kuhusu uhalifu wa Sangoma walionaswa kwa kufanya ngono na wake wa vigogo.

Uchunguzi uliofanywa na waandishi wetu kwa baadhi ya wanawake  hao umebaini kuwa,  waume wao wanafanya kazi  katika nyadhifa za  juu serikalini, wengine ni wastaafu  na kwamba waume hao  hawajui kinachoendelea.
Kwa mujibu wa mwanamke mmoja (jina lipo), katika sakata hilo kuna wake wa maprofesa, kanali mstaafu wa JWTZ na mmoja ambaye mume wake aliwahi kuwa kamanda wa polisi wa mkoa (RPC) ambaye kwa sasa naye ni mstaafu.
...Kamanda Kiondo akizidi kuonyesha vifaa vilivyokuwa vikitumiwa na waganga hao wa kienyeji.

Mwanamke huyo alizidi kudai kuwa, ndoa moja katika hizo ilivunjika baada ya mume kubaini kuwa, mkewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa sangoma hao.
‘KUFULI’ ZILISHATUMIKA

Uchuguzi zaidi ulibaini kuwa zaidi ya nguo za ndani  ‘kufuli’ za  wanawake zaidi ya 20 zilizokutwa  na polisi  kwa sangoma hao maeneo ya Tandika jijini Dar es Salaam zilikuwa zimeshavaliwa hivyo hakukuwa na mpya jambo lilionesha kuwa, zilivuliwa wakati wa tukio linalodaiwa lilikuwa na kutengezea dawa.

Baadhi ya watuhumiwa wa sakata hilo.

KWA NINI WALITOA TAARIFA POLISI?

“Sisi tuliamua kutoa taarifa polisi kwa sababu tumekuwa tukifanya ngono na wale waganga kwa muda mrefu bila kupata ujauzito na mbaya zaidi tulishatumia mamilioni ya pesa  baada ya kuuza mali zetu, zikiwemo nyumba,” alisema mwanamke huyo nje ya kituo cha polisi.

Wanawake hao ambao hawakupenda majina yao  yatajwe kwa kuhofia waume zao kujua, walisema  ni  kweli baadhi yao wamekaa katika ndoa kati ya miaka nane hadi  10 bila kupata watoto wala mimba zilizoharibika.
Kamanda Kiondo akionesha baadhi ya nguo za ndani, 'kufuli' zilizokutwa kama ushahidi kwa baadhi ya wanawake waliofanyishwa ngono na sangoma hao.

Hata hivyo, baadhi yao walirudishiwa fedha zao baada ya Kamanda Kiondo kuwabana waganga hao.
KAULI YA RPC

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi Mkoa wa Temeke chini ya Kamanda, SACP Englibert Kiondo liliwatia nguvuni sangoma wawili wakiwa na matunguli na zana nyingine za kuagulia binadamu.

Kamanda Kiondo akikusanya tunguli zilizotumiwa na waganga hao wahalifu tayari kwa kuzichoma moto mbele ya wahandishi wa habari.

Vitu hivyo viliteketezwa moto kwenye Kituo cha Polisi Temeke mbele ya  waandishi wa habari.

“Ninaamini kuwa kwa vitendo  hivyo  vya kujamiiana ni hatari na huu ni ubakaji, kwani kuna uwezekano wa kuambukizana maradhi  mbalimbali ikiwemo  Ukimwi, kwa hiyo hizi zana nazichoma moto,” alisema  Kamanda Kiondo.

...Tunguli zikiteketezwa kwa moto.

Waliokamatwa katika zoezi hilo ni Juma Mohamed (32) na Abdallah Musa (25) ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo.



“Siwezi kumwacha, nikimwacha nitakuwa sitendi haki”..... Picha pamoja na habari kamili kuhusu binti huyu na mstaa zipo chini ya uchunguzi, Utazipata baada ya kukamilisha uchunguzi kwa pande zote msanii mmoja baada ya mwingine

Wednesday, July 2, 2014


denti mmoja wa chuo kimoja ambacho tusingependa kukitaja jina kwa kuhofia maadili, amejikuta akipata aibu ya mwaka baada ya picha zake za faragha kusambaa kwa kasi ya ajabu mtandaoni , denti huyo anayesoma masomo ya biashara inadaiwa alikusanya kazi ambayo waliachiwa na mwalimu wao sasa kwa bahati mbaya alisahau kuzifuta kwenye frash na ndipo zikasambaa,
hapo
haijajulikana bado zimevujishwa na nani kati ya mwalimu au huyu jamaa tunayekusanya kazi kwake hili ampelekee mwalimu alizungumza rafiki wa karibu wa denti huyo,akome kwani amezoea amewahi kupiga zingine bhana unabisha?
hivi sasa rafiki yangu. hasomi amechanganyikiwa anahofia siku baba yake atakapoziona picha hizo kwani anasema ni mkali mpaka anamuogopa, jamani ushauri tu mabintimsijiachie sana na camera zitawaponza kama huyu dada, ni hayo 

BOFYA PICHA YA UCHI HAPA
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishna Suleiman Kova.


Watu wawili wamekamtwa kwa tuhuma za mauaji ya Sista Clesencia Kapuli (50) wa Kanisa Katoliki,  aliyekuwa Mhasibu katika Shule ya Sekondari Mwenyeheri, jijini Dar es Salaam.


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema watu hao ni kati ya watu wanane waliokamatwa kwa tuhuma za ujambazi sugu wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema watu hao walikamtwa juzi  katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo kwa kutumia vikosi maalum.

Alisema licha ya majambazi hao wawili kuhusika katika tukio la mauaji ya sista huyo, lakini pia walihusika katika tukio la kupora fedha katika benki ya Barclays tawi la Kinondoni miezi michache iliyopita.

Aliwataja waliohusika hao wa  mauaji ya Mtawa kuwa ni Manase Ogenyeka (35), mkazi wa Tabata na Hamis Ismail, mfanyabisahara na mkazi wa Magomeni Mwembechai.

Watuhumiwa wengine ni Beda Mallya (37), mkazi wa Mbezi Msakuzi; Michael Mushi (50), mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Makabe; Sadick Mohamed (32), mfanyabiashara, mkazi wa Mbagala Kizuani; Elibariki Makumba (30); Nurdin Suleiman (40), wote wakazi wa Buguruni Madenge, pamoja na Mrumis  Saleh (38), mkazi wa Kigogo Freshi.

Pia Jeshi la Polisi limesema linaendelea na operesheni hiyo pamoja na kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio la maujai ya  sista Kapuli, Juni 23, mwaka huu, pamoja na jambazi mmoja aliyehusika katika tukio la wizi wa fedha katika benki ya Barclays. 

Sista huyo ambaye  alikuwa mhasibu wa Shule ya Sekondari Mwenyeheri iliyopo Makoka wilayani Kinondoni, aliuawa Juni 23, mwaka huu  kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazio waliokuwa katika pikipiki aina ya Boxer.

Sista Kapuli alivamiwa na majambazi hao baada ya kutoka benki Mlimani City akiwa katika gari aina ya Pick up double cabin yenye namba za usajili T 213 CTZ.


via>>Nipashe

Wednesday, April 30, 2014

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhoenz2TRKymYQ_Vr_RIrKHmcZ0T2OEkTs1p1Z3mYFtaWCttkDLHnHshCtfBskXQ-aGmNuXr2Mie_Y_0hpjXi3dlZcl3laCqzwL57HU4TDbBODAanBJ4m1MPU3dWV3xqrjMgu1ZN-79VTtX/s1600/AJALI+YA+BASI+LA+SUMRY+DAR-MNZ+BARABARA+KUU+DODOMA-MOROGORO+PIX+NO+5.JPGWATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida jana usiku.
 
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo. 
 
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida. 
 
Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Sunday, March 30, 2014

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi na mmoja kujeruhiwa vibaya wakati wakifanya kibarua cha kushusha nguzo za kusambazia nishati ya umeme vijijini kupitia kampuni ya moja  ya Derm katika kijijini cha Bisumwa wilayani Butiama mkoani Mara.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo  wamesema tukio hilo limeokea leo saa 3.30 asubuhi katika kijiji cha Bisumwa wilayani Butiama,ambapo vibarua hao kutoka kijiji cha sabasaba baada ya kufika kijijini hapo na lori  hilo aina ya Scania yenye namba za usajili T 787 CUL  wakiwa juu ya sheena hiyo ya nguzo na wakati wajaribu kufungua mikanda kwa ajili ya kuzishusha nguzo hizo zilishuka kwa kasi kubwa sambamba na wao hatua ambayo imesababisha watu wawili kufariki dunia kwa kugongwa na nguzo hizo huku wengine wakipata majeraha makubwa yakiwemo ya kuvunjika kwa miguu.
Viongozi wa halmashauri ya Butiama wakiongozwa na mwenyekiti wake Bw Magina Magesa, ambao walifika muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea kwa ajili ya kutoa msaada kwa majeruhi hao,pamoja na kutoa pole  lakini wametaka kampuni zinazohusika kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vya mkoa wa Mara kuchukua tahadhari wakati wa kusafirisha nguzo hizo ili kuepuka ajali mbaya kama hiyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Paul Kasabago, akizungumza na ITV kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa ni Masui Magibo (20) na Salabanze John (22) wote wakazi wa kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama na kwamba majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara mjini Musoma kwa ajili ya matibabu zaidi.
DUKA la kuuza Rasta za wakina Dada (Urembo) limevamiwa na watu waliosadikika kuwa majambazi, Ni muda mchache uliopita kutoka sasa tangu tukio hilo lijiri maeneo ya Kariakoo jijini Dar Es Salaam..
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ni kwamba majambazi waliojaribu kufanya jaribio hilo baadhi yao wameuwawa na baadhi, Idadi kamili endelea kufatilia hapa maana waandishi pamoja na wadau bado wapo katika eneo la tukio kufatilia kwa kina.

Saturday, March 29, 2014


Njemba moja ambaye jina lake halikuweza kufahamika kwa mara moja amekutwa na dhahma kubwa ya mwaka. Dhahma hiyo ya kuvuliwa nguo zote na kutembezwa maeneo mbalimbali ya Jiji la dar es salaam ilimkuta baada ya kufumaniwa akitembe na mke wa mdosi. www.gwijilahabari.blogspot.com
 

Jamaa akiwa ndani ya gari maeneo ya bank ya NBC huku watu wakimshangaa na kuhamaki.
 








Thursday, March 27, 2014

AIBU! Wakati Wakristo bado wapo kwenye Kwaresma, mama aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, amenaswa laivu akijiuza maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 24, mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina wakiwemo mabinti wadogo. 
Chanzo hicho kilimwaga data kuwa, kuna mzee maarufu kwa jina la babu katika eneo hilo ambaye amekuwa akiwapa machangudoa hifadhi katika banda lake na kuwapa magodoro chakavu kwa malipo ya shilingi elfu moja kwa kila kichwa. 
KISIKIE CHANZO
“Jamani kwenye danguro hili kila aina ya uchafu upo. Wanatukwaza sisi Wakristo ambao tupo katika kipindi hiki cha Kwaresma,” kilitiririka chanzo hicho cha kuaminika maeneo hayo. 
OFM KAZINI
Ili kujiridhisha na taarifa hizo, makamanda wawili wa OFM walitimba katika danguro hilo wakajifanya wateja ambapo walimchukua mmoja na kubaini kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi.

Mwalimu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi.
TUJIUNGE NA CHANGU MWALIMU
“Kaka ongea fasta nipe changu, usinione hivi mimi ni mwalimu wa msingi, mshahara haukidhi halafu isitoshe serikali haijatulipa malimbikizo yetu, watulipe bwana pengine tunaweza kujikwamua,” alisema changu huyo ambaye alimtaka kamanda wa OFM alipie shilingi elfu kumi kama malipo ya huduma tendo moja. 
POLISI WAITWA
Baada ya kujiridhisha kwa uwepo wa biashara hiyo, OFM waliwapigia simu polisi wa Kituo cha Kizuiani, wakafika na kufanikisha zoezi la kuwakamata machangu wapatao 16 pamoja na babu anayewapa hifadhi ili wauze miili.

...Wakiingizwa kwenye gari la polisi.
VIBANDA KIBAO VYABAINIKA
Wakati zoezi la kuwakamata likiendelea maeneo hayo, vilibainika vibanda vingi  ambavyo machangu hao hufanyia uchafu wao pamoja na mfuko mkubwa ambao madadapoa hao huhifadhia nguo zao za heshima kabla hawajaingia ‘mzigoni’.
 
WAACHA WATOTO NYUMBANI
Baadhi ya machangudoa hao waliotiwa mikononi mwa polisi, walikiri kuwa wamewaacha watoto wao nyumbani huku wengine wakidai ni wake za watu hivyo kuomba wasipigwe picha kukwepa aibu pindi zitakapochapishwa gazetini.

Watuhumiwa wakiwa kwenye gari la polisi chini ya ulinzi mkali.
“Jamani msitupige picha sisi wengine tuna watoto na waume zetu, tunaomba msamaha jamani,” walisikika madadapoa hao.
 
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya kamatakamata kukamilika, machangu hao pamoja na mzee huyo walipandishwa kwenye difenda la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kizuiani kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka ya uzururaji.

Wednesday, March 19, 2014

Hakika pengine ukiangalia picha hizi unaweza dhani kuwa ni picha za kutengeza lakini ni hali ya kweli hawa wameungana lakini wanafanya kazi nyingine kama kawaida ikiwa pamoja na kufanya shughuli za kimuziki wana uwezo wa kupiga kinanda tunafanya jitihada ya kutafta video lakini kwa sasa angalia picha zaidi kumbuka licha ya kuwa na ulemavu huo lakini vijana hawa wanapiga kazi kama nini

Tuesday, March 18, 2014

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.




Joseph Mwaisango wa Mbeya yetu akiwa amempakata mtoto huyo

Baadhi ya waandishi wa habari wakiongea na mama mkubwa wa mtoto huyo


MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.
 
Akizungumza kwa masikitiko Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.
 
Anasema tukio hilo lilitokea Mwaka jana Mwezi wa Nane lakini alipopatiwa matibabu katika kituo cha afya mtoto huyo aliungana ngozi ya kidevu na kifua hali inayomletea shida ya kula na kufurahi na wenzake.
 
Anasema tangu kipindi hicho alimchukua mtoto huyo kwa mama yake na kuanza kuomba msaada wa matibabu baada ya kumpeleka katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Makete Mkoani Njombe ambapo Wataalamu walimwambia atafute Shilingi Milioni Moja ili mtoto wake aweze kutibiwa.
 
Ameongeza kuwa baada ya muda wataalamu hao walimwambia asubiri Wazungu kutoka Ulaya ambao wataweza kumtibia mwanaye ambapo baada ya kusubiri kwa muda kidogo Wazungu hao walifika na kumcheki Mwanaye kisha kumwambia wao hawana utaalamu isipokuwa aende CCBRT Dar Es Salaam ambako ataweza kutatuliwa tatizo lake.
 
Aidha kutokana na kuambiwa hivyo Mama huyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kumpeleka Mtoto wake kwa matibabu kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuweza kusafiri hadi DSM pamoja na gharama za matibabu kuwa kubwa.
 
Amesema anahitaji zaidi ya shilingi Milioni 2 ili ziweze kumsaidia kusafiri kugharamia matibabu pamoja na huduma za Kawaida kipindi atakachokuwepo Jijini Dar Es Salaam wakati akisubiri matibabu ya Mwanaye.
 
Mtu yeyote mwenye kuguswa na tatizo hilo anaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mama huyo kupitia simu yake ya Mkononi namba 0752 986879 au Nyumbani kwake Iyunga Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya.

Sunday, March 9, 2014

CHEKI VIDEO HIYO HAPA



Na.Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya 21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP amewataja watu hao kuwa ni:

1. VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23, Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.
2. ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30, Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.

3. MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26, Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.

4. REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka 38, Mlugulu mkazi wa Airport Morogoro.

5.JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22, Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.

6. FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20, Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.

7. BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27, Mkurya mkazi wa Tarime Mara.

8. SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23, Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.

9. ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28, Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.
10. SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.

11. HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31, Mnyamwezi mkazi wa Urambo Tabora.

12. AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38, Mbulu mkazi wa Babati Manyara.

13.JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka 31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.

14.DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29, Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.

15.DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23, Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.
Aidha Kamanda MISIME amesema katika msako huo watu wawili wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane (8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.
Pia huko katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.
Kamanda MISIME amesema msako unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi 

Click here

Click here

Popular Posts