Showing posts with label BREAKING NEWS. Show all posts
Showing posts with label BREAKING NEWS. Show all posts

Sunday, March 30, 2014

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine kumi na mmoja kujeruhiwa vibaya wakati wakifanya kibarua cha kushusha nguzo za kusambazia nishati ya umeme vijijini kupitia kampuni ya moja  ya Derm katika kijijini cha Bisumwa wilayani Butiama mkoani Mara.
Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo  wamesema tukio hilo limeokea leo saa 3.30 asubuhi katika kijiji cha Bisumwa wilayani Butiama,ambapo vibarua hao kutoka kijiji cha sabasaba baada ya kufika kijijini hapo na lori  hilo aina ya Scania yenye namba za usajili T 787 CUL  wakiwa juu ya sheena hiyo ya nguzo na wakati wajaribu kufungua mikanda kwa ajili ya kuzishusha nguzo hizo zilishuka kwa kasi kubwa sambamba na wao hatua ambayo imesababisha watu wawili kufariki dunia kwa kugongwa na nguzo hizo huku wengine wakipata majeraha makubwa yakiwemo ya kuvunjika kwa miguu.
Viongozi wa halmashauri ya Butiama wakiongozwa na mwenyekiti wake Bw Magina Magesa, ambao walifika muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea kwa ajili ya kutoa msaada kwa majeruhi hao,pamoja na kutoa pole  lakini wametaka kampuni zinazohusika kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vya mkoa wa Mara kuchukua tahadhari wakati wa kusafirisha nguzo hizo ili kuepuka ajali mbaya kama hiyo.
Kaimu kamanda wa polisi wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Paul Kasabago, akizungumza na ITV kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu kuwa ni Masui Magibo (20) na Salabanze John (22) wote wakazi wa kijiji cha Sabasaba wilayani Butiama na kwamba majeruhi wote wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara mjini Musoma kwa ajili ya matibabu zaidi.
DUKA la kuuza Rasta za wakina Dada (Urembo) limevamiwa na watu waliosadikika kuwa majambazi, Ni muda mchache uliopita kutoka sasa tangu tukio hilo lijiri maeneo ya Kariakoo jijini Dar Es Salaam..
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ni kwamba majambazi waliojaribu kufanya jaribio hilo baadhi yao wameuwawa na baadhi, Idadi kamili endelea kufatilia hapa maana waandishi pamoja na wadau bado wapo katika eneo la tukio kufatilia kwa kina.

Saturday, March 8, 2014

Daktari akiwa amezamisha kidole chake kwenye jeraha la Ndugu Richard wakati alipokuwa akimsafisha kidonda baada ya tukio hilo.
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga, kwa taarifa zisizo rasmi zinasema Wanaodhaniwa ni Vijana wa CCM  wamchoma kisu cha Mbavu Ndugu Richard ambaye ni M/Kiti wa Tawi la CHADEMA la Kijiji cha Tagamenda siku moja tu baada ya Mama Mzazi wa Kijana huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuamua kuhamia CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na siasa zisizokuwa na mwelekeo za Chama hicho!!!!

Sunday, March 2, 2014

Mtangazaji wa Channel Ten, Salum Mkambala (pichani) amepata ajali ya gari ambalo alikuwa akiendesha kutoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro. Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Channel Ten ambaye ameidokeza Global Publishers.info,

Saturday, March 1, 2014

Poleni vijana. Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM, kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”

Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.

Wednesday, February 5, 2014


Manyara, Tanzania. Ndege ya iliyokuwa imebeba madaktari wanne 'Flying Doctors' imeanguka katika, mkoani Manyara baada ya kupata hitilafu wakati ikijiandaa kupaa kuelekea vijijini.

Ndege hiyo ilikuwa vijiji vilivyopo Kata ya Ndedo wilayani Kiteto, mkoani Manyara kwa ajili ya kutoa huduma ya mama na mtoto.

Daktari mmoja amejeruhiwa na wengine wanaendeleo vizuri.
Blog ya wananchi

Click here

Click here

Popular Posts