Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Friday, July 11, 2014

Screen Shot 2014-07-11 at 9.14.30 AMIfuatayo ni kauli ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa Bumbuli Tanga kuhusu Naibu waziri ambae pia ni mbunge wa Bumbuli January Makamba.
Amenukuliwa akisema >>> ‘January anafanya kazi nzuri ya ubunge pia ananisaidia sana kwa kazi ya wizara niliyompa, unajua January alipogombea Ubunge alinificha nilikuwa nasikia kwa wenzake tu pale ofisini, baadae alivyoweka mambo yake sawa ndio akaja kuniambia kwamba Mzee na Mimi najitosa’
‘Nikamtakia heri… kwa kweli kwa jinsi anavyohangaika na Jimbo lake inaonyesha Ubunge aliutaka kwa dhati kabisa ya kusaidia watu wa Bumbuli, nimesikia anafikiria mambo makubwa… hajaniambia mi nimesikia tu, namtakia kila la heri…. haya mambo anaamua Mungu wala hayalazimishwi’
Screen Shot 2014-07-11 at 8.53.32 AM
‘Mungu akitaka linakuwa hata kama watu wote hawataki, Mungu akiwa hataki hata kama mtu ukitaka jambo hilo vipi haliwezi kuwa, mimi nilishauriwa na Mzee mmoja kwamba jambo likifika wakati wake utalipata hata kama utapingwa kiasi gani, kama halijafika wakati wake haliwezi kutokea, mimi niligombea 1995 sikupata kwasababu haikuwa wakati wake…. 2005 ikawa wakati wake nikapata, na wewe usipopata sasa usiweke nongwa” – JK

Wednesday, March 19, 2014



Mbunge wa Viti Maalum wa Chadema, Rose Kamili amedai kupigwa na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati walipomkamata na kumshikilia kwa muda kwa tuhuma za kutoa rushwa. 
 
Mbunge huyo kwa sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa akitibiwa majeraha yake na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kwa sasa wanasubiri taarifa ya uchunguzi ili kuamua kama ahamishiwe Hospitali ya Taifa ya Muhimbili au KCMC.

 
“Wamenipiga, wamenidhalilisha vya kutosha,” alisema mbunge huyo huku akitokwa na machozi. “Walipanua miguu yangu na kunikanyaga sehemu za siri. Kama angekuwa mwanamume sijui angekuwa katika hali gani?”
 
Alisema vitendo hivyo vilifanywa na walinzi wa CCM, wanaojulikana kwa jina la Green Guard, ndani ya ofisi ya chama hicho Mkoa wa Iringa na vilishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Iringa, Jesca Msambatavangu.
 
Muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana, Kamili aliliambia  Gazeti la Mwananchi  kwamba wafuasi wa CCM walimteka wakati akitoa maelekezo kwa mawakala wa Chadema waliokuwa wamepangwa kusimamia uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga.
 
Mbunge huyo alisema aliporwa Sh350,000, Pauni 500 za Uingereza, simu mbili; moja aina ya Nokia na nyingine Samsung, pamoja na nakala 16 za daftari la wapigakura ambazo walikuwa wapewe mawakala waliokuwa kwenye mkutano.
 
Wakati kukiwa na tuhuma utekaji uliofanywa na wafuasi wa CCM, Msambatavangu alikiri jana kuwa chama hicho tawala kilimshikilia kwa lengo la kumuhifadhi hadi polisi walipofika, lakini akakanusha madai ya kuhusika kwa wafuasi wa CCM katika tukio hilo.
 
“Siyo kweli. Ni madai ya uongo na kama anadai hivyo tusubiri uchunguzi wa polisi ili ukweli ujulikane,” alisema Msambatavangu.
 
Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi alikiri kuwa polisi walimkuta Kamili kwenye ofisi za CCM za mkoa na kwamba waliondoka naye baada ya kupewa taarifa na makada wa chama hicho kwamba alikutwa akitoa fedha.
 
“Askari wetu waliokuwa kwenye msafara wa mgombea wa CCM waliporudi, maana ilikuwa jioni, walimkuta huyo mtuhumiwa akiwa kwenye ofisi za chama hicho ndipo walipompeleka kituoni,” alisema.
 
“Tuliambiwa amekutwa akitoa rushwa, lakini alipofika kituoni naye akadai kwamba alitekwa, kupigwa na kudhalilishwa. Sasa tumefungua majalada ya kuchunguza tuhuma zote mbili – suala la rushwa na madai yake ya kutekwa.”
 
Kamanda Mungi alisema polisi hawafahamu mbunge huyo alikaa kwa muda gani kwenye ofisi za CCM kabla ya wao kumchukua.

Kuhusu ushiriki wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika suala hilo, Mungi alijibu: “Kazi ya polisi ni ya polisi na ya Takukuru ni ya Takukuru, kama unataka kujua kuhusu wao pengine ukawaulize.”
 
Hata hivyo, Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Iringa, Emma Kuhanga aliwaongoza maofisa wake kwenda polisi kuitika wito wa Kamanda Mungi aliyewaarifu kuwepo kwa mtu aliyekamatwa kwa rushwa.
 
Jana Kamanda Kuhanga alikiri kuitwa polisi lakini akasema: “Ndiyo tulikwenda polisi, lakini tumeshindwa kushiriki kwenye mchakato wa tuhuma hizo kwa sababu hatukupata maelezo yanayoeleweka.”

 
Alazwa hospitali
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma jana alizuiwa na walinzi wa Chadema kumwona Kamili alipokwenda kumjulia hali hospitalini.
 
Kuhusu tuhuma za rushwa, Msambatavangu alisema wanakijiji waliizingira nyumba ambayo walihisi kwamba Kamili alikuwa akigawa fedha na kuivamia kwa lengo la kuwakurupusha.
 
“Kwa kuwa baadhi ya vijana wetu walikuwa eneo hilo, sisi tulichukua jukumu la kumpandisha haraka kwenye gari letu na tulikimbia haraka maana tungemwacha pale wananchi wangemuumiza,” alisema Msambatavangu ambaye alisema gari la Chadema lilifika eneo hilo na kuzuia njia lakini wakafanikiwa kuondoka naye. ambaye alisema kundi la wafuasi wa CCM wakiongozwa na Green Guard walivamia mkutano wa ndani wa Chadema ambao ulikuwa ukiwapa mawakala maelekezo jinsi ya kusimamia uchaguzi.
 
“Walikuwa wamemlenga mbunge yaani mimi, walipotuvamia ilizuka taharuki na kunibeba na kunipandisha kwenye gari kwa nguvu, ndani ya gari walikuwa wanaume tu na idadi yao ilikuwa ni 13,” alisema Kamili na kuongeza:
 
“Wakati gari linataka kuondoka, gari letu la M4C lilizuia njia, na waliokuwa ndani ya gari waliambizana kwamba pita porini hata tukipata ajali sawa tu…wakapita porini na walikimbia sana hadi CCM mkoa ambako walianza kunitesa”.
 
Mbunge huyo alisema walipokuwa wakimpiga walikuwa wakisema kwamba lazima wawakomeshe wabunge wa Chadema. “Waliniuliza umekuja kufanya nini huku, kwani huku ni kwenu Manyara?...wakasema lazima tuwakomeshe wabunge wa Chadema na hata kama ni kuua mmoja ili mkome”.
 
Kamili alisema aliokolewa na polisi ambao walifika katika ofisi hizo na kumchukua kwa mahojiano ambayo yalifanyika hadi saa 6:09 usiku wa kuamkia jana.


 
 
 

>>Mwananchi

Saturday, March 8, 2014

Daktari akiwa amezamisha kidole chake kwenye jeraha la Ndugu Richard wakati alipokuwa akimsafisha kidonda baada ya tukio hilo.
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kalenga, kwa taarifa zisizo rasmi zinasema Wanaodhaniwa ni Vijana wa CCM  wamchoma kisu cha Mbavu Ndugu Richard ambaye ni M/Kiti wa Tawi la CHADEMA la Kijiji cha Tagamenda siku moja tu baada ya Mama Mzazi wa Kijana huyo ambaye alikuwa Mjumbe wa Serikali ya Kijiji hicho kwa tiketi ya CCM kuamua kuhamia CHADEMA kwa madai ya kuchoshwa na siasa zisizokuwa na mwelekeo za Chama hicho!!!!

Thursday, March 6, 2014

Hapa duniani kwasasa kuna mabilionea 1645 , kutokana na takwimu zilizotolewa na Forbes. Kwa mwaka jana bara la Afrika lilikua na mabilionea 20 lakini kwa mwaka huu wameongezeka mabilionea 9 na mmoja wapo ni mtanzania. Kwa upande wa sanaa ya hapa Bongo basi tunaweza kusema Diamond na Lady jaydee ndio wanaongoza kwa mkwanja labda ni kwasababu ya uwekezaji wao wanaofanya na kila kukisha kutuonesha mapesa na magari wanaomiliki lakini sio mbaya ukamjua tajiri namba moja Tanzania na namba mbili kwa Afrika mashariki akiachwa na Sudhir Ruparelia kutoka Uganda mwenye utajiri wa bilioni  1.1 za kimarekani .
Anaitwa Rostam Aziz, 53 ndio bilionea pekee Tanzania. Anamiliki asilimia 35 ya mtandao wa Vodacom, Mtandao mkubwa zaidi nchini wenye watumiaji zaidi ya millioni 10.Pia Rostam anamiliki mgodi wa Caspian Mining.pia anamilikia asilimia fulani kwenye bandari ya Dar-es-salaam. Na pia anafanya biashara za nyumba nchi za Tanzania, Dubai, Oman and Lebanon. Rostam ana utajiri wenye thamani ya bilioni 1 za kimarekani.
Rostam-Aziz-Forbes-vibe-co-tz
Ikumbukwe kwamba Akon ndio msanii tajiri kuliko wote Afrika na utajiri wake ni dola za kimarekani milioni 80 na kwa mwaka huu ameanza kampeni ya kuzipa mwanga nyumba zaidi ya milioni moja katika nchi za afrika magharibi na afrika ya kati.
Akon
Tujiulize ni lini wasanii wa kibongo watafika level kama alizofika Akon na sio kwa kipato bali kwa ile hali ya kurudisha shukrani kwa jamii na kuacha kuturingishia utajiri wao.

Tuesday, March 4, 2014

Frederick Mwakalebela akiwa na raisi JK
MWANASIASA na  mdau wa soka kijana,  Frederick Mwakalebela ametabiri kuwa ikiwa malumbano ndani ya Bunge Maalum la Katiba linaloketi mjini Dodoma litaendeleza malumbano ya makundi, bunge hilo litaongezewa muda na hata kusababisha Uchaguzi Mkuu wa  2015 kusogezwa mbele.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za gazeti hili Bamaga Mwenge jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwakalebela alisema makundi ndani ya Bunge Maalum la Katiba ni tatizo ambalo anaamini Rais Jakaya Kikwete atakapolifungua rasmi hilo atalizungumzia.

Baadhi ya mahojiano kati ya Mwakalebela na waandishi wa Global ni haya yafuatayo:

Mwandishi: Makundi yameibuka bungeni, wewe ungewashauri nini wajumbe wa bunge hilo?
Mwakalebela: Ni kweli nafuatilia na hata mimi nimeliona hilo la makundi. Wajumbe wakiendeleza malumbano ya kimakundi, naamini muda waliopewa wa siku 70 hautatosha na wataongezewa siku 20 na kuwa 90. Lakini malumbano ya kimakundi nilikuwa naamini CCM (Chama Cha Mapinduzi) watakuwa kitu kimoja lakini humo namo kuna wanaopingana.

Wajumbe wale 600 waelewe kuwa wapo pale kutuwakilisha sisi zaidi ya milioni 44 tulio nje, wajue kuwa wao ni wawakilishi tu.

Naamini Rais Jakaya Kikwete atakapowahutubia wakati wa ufunguzi atawaeleza hilo na atawahimiza wawe wamoja kwani jukumu kubwa la kupata katiba mpya tumewaachia wao.

Mwandishi: Mwaka 2010  wakati wa uchaguzi mkuu ulipokuwa ukigombea Ubunge Jimbo la Iringa Mjini ulikumbwa na kashfa ya kutoa rushwa kabla ya mahakama kukuona huna kosa. Unaweza kueleza ilikuwajekuwaje yakatokea yale?

Mwakalebela: Ni kweli mwaka ule upepo wa kura za maoni kwa upande wa chama changu (CCM) ulikuwa kwangu, lakini baadaye nilishitukia nikiambiwa niende nikatoe maelezo kwenye vyombo vya serikali nikayakuta hayo. Lakini kama mjuavyo mahakama iliniona sina hatia na nikaachiwa huru.

Mwandishi: Je, baada ya kutokea zahama hiyo, unasemaje kuhusu mwaka 2015, utagombea?

Mwakalebela: Kanuni za chama changu haziruhusu kwa sasa mtu kutangaza kugombea lakini niseme tu kwamba natamani kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa mwakani.

Ni kwamba katika maisha yangu nimesaidia watu wengi sana kulingana na uwezo wangu na wananchi wanapenda nivae koti la uongozi wakiamini kwamba nitasaidia zaidi ya hivi ninavyofanya sasa.

Mwandishi: Kabla ya kuingia katika siasa ulikuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ukafanya vizuri kiuongozi, unaweza kutaja changamoto za wakati ule pale?

Mwakalebela: Nilikumbana na changamoto nyingi. Nakumbuka siku ya kwanza Rais wa TFF (wakati ule), Leodiger Tenga aliponitambulisha, makomandoo wa pale walisema huyu unayetuletea si mtu wa soka bali ni mwimbaji wa kwaya eti kwa sababu nilikuwa nimevaa tai. Sijui walitaka nivaaje. Lakini changamoto mojawapo ilikuwa ni kuhusu fedha zilizotokana na mapato ya milangoni.

Nilisema tuzitangaze ili wadau wajue. Tukawa tunafanya hivyo lakini wananchi wakawa hawaridhiki na tunachotangaza. Baadaye tulifanya kazi na viongozi wenzangu wa TFF wakati ule, ushirikiano na serikali ukawa mkubwa kuanzia kwa Rais Kikwete na mawaziri waliokuwa wakihusika na michezo, Seif Khatibu, Joel Bendera na baadaye Amos Makalla walituunga mkono sana.
Mwandishi: Licha ya soka na siasa kuna mengine unayoyafanya kitaifa?

Mwakalebela: Ndiyo, kwa sasa mimi ni Mtawala Mkuu wa Makumbusho ya Taifa na tumekuwa tukijitahidi kufanya kitengo hicho kinufaishe taifa.Tunataka ifanyiwe matangazo.

Hivi sasa wananchi,watu kutoka nje ya nchi wanakuja kuangalia Makumbusho ya Taifa na tunaingiza kama dola za Kimarekani 300,000 kwa mwaka.

Monday, March 3, 2014



Ever since the evolution of man-kind, there has always existed this peculiar rage & urgency in our race to prove one’s dominancy upon the other. We all know that in ancient gladiator times power was determined by the size of the army and their ability to win wars, well has it changed that much? We humans seem to be caught in a never-ending war between ourselves whereas the beneficiaries never have done or will do any of the dirty work and just control everything from behind the scenes. The Oxford dictionary describes the act of war as a, ‘’ state of armed conflict between different countries or different groups within a country.’’
The following list is not in a chronological order, instead is sorted from the war with the lowest death toll to the highest. So here, we have the world’s ten biggest bloodiest wars in history.

 10. American Civil War (1861-1865)

american civil war 1 World’s Top Ten Biggest Wars in History
The American Civil War was basically a war fought between the ‘North’ or the ‘Union’ and the South also known as the ‘Confederacy’ formed by the secession of several southern slave states. It was also known as the War Between the States or simply just the Civil War. The war had its roots set on issues of slavery and the extensions of it into the western territories of America. More than 800,000 people were killed in the war.

 9. Soviet War in Afghanistan (1979-1989)

Soviet War Afghanistan12 World’s Top Ten Biggest Wars in History
A decade long war between the Soviet-led Afghan forces and the multi-national insurgent groups called the Mujahedeen; with the death toll of well over a million Afghan civilians and those that were participants in the war. The war although fought only in Afghanistan, billions of dollars were funded by countries like the United States, United Kingdom, Saudi Arabia and a few other.

8. Vietnam War (1955-1975)

vietnam war 02 World’s Top Ten Biggest Wars in History
Also known as the Second-Indochina War and as this period of American involvement in Vietnam made it the American War was basically a sequel to the First Indochina War that was fought between North Vietnam – supported by China and other communist allies and South Vietnam – supported by the United States and other anti-communist allies. Over a million civilians were killed in addition to the hundreds of thousands participants in the war.

7.  Thirty Year’s War (1618-1648)

thirtyyearswars World’s Top Ten Biggest Wars in History
One of the bloodiest wars on religion, as the name suggests itself a war that lasted over three decades; Thirty Year’s War was one of the longest and the most destructive conflicts in the European history and one of the longest continuous wars in Modern history. Historians have still not come to terms on the fact as to what ignited the fighting; rather there seem to be many parallel causes that fueled the war overtime. It grew as a religious war at first, but then developed into a continuation of the Bourbon-Habsburg rivalry for the European political pre-eminence with the death toll of well above 5 million people.

6. Napoleonic Wars (1803-1815)

napoleonic wars World’s Top Ten Biggest Wars in History
Napoleonic Wars were a series of wars declared against the Napoleon’s French Empire by the opposing coalitions. The war was initially sparked by the French Revolution of 1789 and played out on an unprecedented scale, mainly owing to the application of modern mass conscription. French power was stronger than ever as Napoleon armies had conquered much of Europe but came to an ultimate military defeat after France’s disastrous invasion of Russia in 1812. With over six and a half million people dead the war came to an end resulting in the restoration of the Bourbon-Monarchy in France and the creation of the Concert of Europe.

5. Russian Civil War (1917-1922)

civil war russia moscow World’s Top Ten Biggest Wars in History
A war fought between the Bolshevik Red Army and the White Army, the loosely allied anti-Bolshevik forces; in the former Russian Empire was in fact a multi-party war with notably many foreign armies like the Allied Forces and pro-German armies warring against the Red Army. The war lasted only five short years but resulted in the death of over 7 million people all in all.

4.  Conquests by the Empire of Japan (1894-1945)

Conquests by the Empire of Japan World’s Top Ten Biggest Wars in History
The Empire of Japan literally means the empire and world power that had existed from the Meiji Restoration that happened on 3rd January 1868 to the enactment of the post World War II Constitution of Japan on 3rd May 1947. Only after suffering a couple defeats and the atomic bombings of Hiroshima and Nagasaki did the Empire of Japan surrendered to the Allies on the 2nd of September, 1945. The American involvement gave birth to a new constitution and was forced on from 3rd May, 1947 officially dissolving the Empire which had already been the cause of over 20 million deaths.

3. World War I (1914-1918)

world war 1 World’s Top Ten Biggest Wars in History
World War I was one of the bloodiest global wars in the history of man-kind centered in Europe that began on 28 July 1914. It was previously called the Great War from its occurrence until the start of the mother of all blood baths in history, World War II. It involved all the great powers in the world, assembled in two opposing alliances the Allies and the Central Powers. The death toll for World War I was estimated to be around a staggering 50 million plus.

2.  Mongol Conquests (1206-1368)

Mongolia empire World’s Top Ten Biggest Wars in History
A war that sparked in the dawn of the 13th century which resulted in the vast expansion of the Mongol Empire that covered much of Asia and Eastern Europe by mid 1300. It is believed by many historians that Mongol raids and invasions were one of the deadliest conflicts in human history up through that period. The Mongols brought terror to Europe on a scale not ever seen again until the twentieth century with more than 60 million killings on their way.

 1.  World War II (1939-1945)

world war 2 World’s Top Ten Biggest Wars in History
Also known as the Second World War, fought between the vast majority of the world’s nations – including all the great powers – eventually forming two opposing military alliances like the First World War; the Allies and the Axis. Marked by mass deaths of civilians, including the Holocaust and the only use of nuclear weapons in warfare up to present, the war resulted in over 70 million fatalities and is believed to be the deadliest, bloodiest war ever in history which shook forever the foundations of our own existence.

Final Conclusion: Although these wars were fought on different territories by various groups and countries on different time periods in history; the ones who always suffered and lost were the same innocent civilians. Never in the field of human conflict was so much owed by so many to so few, like in these pointless wars for blinding power. Albert Einstein was once asked by a reporter after the World War II had ended, ‘’Sir what type of machinery and weapons do you think will be used in the World War III?’’ He answered with a smile, ‘’I don’t know about the World War III but if there is a World War IV, then it will surely be fought with sticks and stones.’’

Saturday, March 1, 2014

Poleni vijana. Taarifa iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mwanga Kilimanjaro Ndugu Japhar Mghamba na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu wilaya ya Dar es salaam Ndugu Daniel Zenda wameshambuliwa kwa Risasi na watu wasiojulikana.
Viongozi hao ambao wapo wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kwenye operesheni maalum inayojulikana kama operesheni Kokoro ambayo inalenga kuhamasisha vijana wa upinzani na wasio na vyama kujiunga na CCM, kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu, na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kauli mbiu ya “..CCM Mwanga Ukimya sasa Basi..”

Viongozi hao wa Jumuiya na Chama cha Mapinduzi wamekumbwa na Mkasa huo wa kusikitisha wakiwa wamemaliza sehemu ya kwanza ya Ziara hiyo katika Kata ya Kisangara na wakirejea mwanga mjini, Kwa bahati Njema hakuna aliyepoteza maisha na tayari taarifa zimesharipotiwa kituo cha Polisi Mwanga ambapo taratibu za Uchunguzi zinaendelea.

Thursday, February 27, 2014

Stori: Hamida Hassan

Picha za nusu utupu ambazo amezipiga mwanamitindo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo zinaonekana kumtesa kufuatia baadhi ya waumini wa kanisa analosali kumsema kuwa anakwenda kinyume na maadili.
Picha hizo anazoonekana amevaa gauni refu jekundu huku likiwa na mpasuo ‘wa haja’ uliyolifanya sehemu kubwa ya paja lake kuwa wazi, zimesambaa kiasi cha kuwafanya baadhi ya mashabiki wake kumtaka ajiangalie upya.
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wadau wamesema kutokana na jinsi alivyokuwa ametulia kiimani, mrembo huyo alikuwa anaelekea kwenye ulokole lakini kwa hili anapotea.
“Unajua yule ni modo mwenye jina kubwa sana lakini alikuwa ametulia sana, hata nilipomuona amejiunga na kwaya ya pale kanisani kwetu St. Peter, niliona ameamua kumfuata Yesu kikwelikweli lakini kwa picha hizi, mh!” alisema Juster John anayesali kanisani hapo.
Naye rafiki wa Jokate aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema: “Ninachokumbuka Jokate aliwahi kuniambia anataka kuokoka ili amtumikie Yesu kisawasawa lakini kwa mavazi haya nadhani mawazo ya ulokole itakuwa basi tena.”
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Jokate na kumuuliza juu ya picha hizo, alipopatikana alisema: “Nilizipiga kwa ajili ya kuitangaza kampuni yangu ya mitindo ya Kidoti.
Ijumaa: Sasa mbona umeacha mapaja wazi sana?
Jokate: Huh!
Ijumaa: Huh nini?
Jokate: Nishasema ni za Kidoti, ilikuwa ni kwa ajili ya kutangaza nguo na nywele zangu.
Ijumaa: Kuokoka ndiyo basi tena?
Jokate: Kimyaaa.
Hata hivyo gazeti hili linamshauri mrembo huyu kwamba, kwa kuwa ameshajijengea heshima kubwa kwenye jamii, ni vyema akawa makini na mavazi kama haya ambayo yanaweza kumfanya akatafsiriwa tofauti.
credit: gpl

Wednesday, February 26, 2014


Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.PICHA|MAKTABA 
Kwa ufupi
Hoja ya kutaka nyongeza ya posho iliibuliwa na wajumbe wawili ambao pia ni wabunge wa CCM, Richard Ndasa (Sumve) na Suleiman Nchambi (Kishapu).
Dodoma. Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.
Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.
Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono.
“Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao,” alisema.
“Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo,” alisema.
Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka. Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa.
Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo.
Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.
Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti serikalini.
“Siku zote ukweli unauma. Nasema kama kuna mjumbe ambaye anaona huko alikokuwa kabla ya kuteuliwa alikuwa anapata pesa zaidi kuliko hii, basi kwa heshima afungashe virago na kuondoka,” alisema.
Via Mwananchi

Click here

Click here

Popular Posts