Thursday, March 27, 2014

AIBU! Wakati Wakristo bado wapo kwenye Kwaresma, mama aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, amenaswa laivu akijiuza maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Mwalimu akiwa ameduwaa baada ya kunaswa kwenye sakata hilo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Machi 24, mwaka huu ambapo awali, wakazi wa eneo hilo waliwatonya mapaparazi wa Operesheni Fichua Maovu (OFM) kuwa kuna danguro kubwa maeneo ya Kizuiani ambalo limesheheni madadapoa wa kila aina wakiwemo mabinti wadogo. 
Chanzo hicho kilimwaga data kuwa, kuna mzee maarufu kwa jina la babu katika eneo hilo ambaye amekuwa akiwapa machangudoa hifadhi katika banda lake na kuwapa magodoro chakavu kwa malipo ya shilingi elfu moja kwa kila kichwa. 
KISIKIE CHANZO
“Jamani kwenye danguro hili kila aina ya uchafu upo. Wanatukwaza sisi Wakristo ambao tupo katika kipindi hiki cha Kwaresma,” kilitiririka chanzo hicho cha kuaminika maeneo hayo. 
OFM KAZINI
Ili kujiridhisha na taarifa hizo, makamanda wawili wa OFM walitimba katika danguro hilo wakajifanya wateja ambapo walimchukua mmoja na kubaini kuwa ni mwalimu wa shule ya msingi.

Mwalimu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi.
TUJIUNGE NA CHANGU MWALIMU
“Kaka ongea fasta nipe changu, usinione hivi mimi ni mwalimu wa msingi, mshahara haukidhi halafu isitoshe serikali haijatulipa malimbikizo yetu, watulipe bwana pengine tunaweza kujikwamua,” alisema changu huyo ambaye alimtaka kamanda wa OFM alipie shilingi elfu kumi kama malipo ya huduma tendo moja. 
POLISI WAITWA
Baada ya kujiridhisha kwa uwepo wa biashara hiyo, OFM waliwapigia simu polisi wa Kituo cha Kizuiani, wakafika na kufanikisha zoezi la kuwakamata machangu wapatao 16 pamoja na babu anayewapa hifadhi ili wauze miili.

...Wakiingizwa kwenye gari la polisi.
VIBANDA KIBAO VYABAINIKA
Wakati zoezi la kuwakamata likiendelea maeneo hayo, vilibainika vibanda vingi  ambavyo machangu hao hufanyia uchafu wao pamoja na mfuko mkubwa ambao madadapoa hao huhifadhia nguo zao za heshima kabla hawajaingia ‘mzigoni’.
 
WAACHA WATOTO NYUMBANI
Baadhi ya machangudoa hao waliotiwa mikononi mwa polisi, walikiri kuwa wamewaacha watoto wao nyumbani huku wengine wakidai ni wake za watu hivyo kuomba wasipigwe picha kukwepa aibu pindi zitakapochapishwa gazetini.

Watuhumiwa wakiwa kwenye gari la polisi chini ya ulinzi mkali.
“Jamani msitupige picha sisi wengine tuna watoto na waume zetu, tunaomba msamaha jamani,” walisikika madadapoa hao.
 
WAFIKISHWA POLISI
Baada ya kamatakamata kukamilika, machangu hao pamoja na mzee huyo walipandishwa kwenye difenda la polisi na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kizuiani kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kufikishwa Mahakama ya Jiji kujibu mashitaka ya uzururaji.

0 comments:

Post a Comment

Click here

Click here

Popular Posts