Ray C ambaye anajipanga kurudi kwa kasi katika muziki wa Bongofleva
anadaiwa kulimezea mate penzi la Diamond Platinumz huku akihaha usiku na
mchana kumpata kwa kumpindua Wema Sepetu ambaye kwasasa ndiye
anayelifaidi penzi la Diamond. ...
Chanzo kimoja kilicho karibu na star huyo kikizungumza na Swahilitz kilisema kuwa kwasasa jina la Diamond halikauki mdomoni mwa Ray C :
"Kwa sasa Ray C haambiwi kitu kwa Diamond, ana haha kila wakati kumweka mikononi mwake, hana furaha kabisa hadi lengo lake litakapotimia, na muda si mrefu mtaandika juu ya hao"
Inadaiwa Ray C amekuwa akipanga miadi ya kuonana na Diamond mara kadhaa bila mafanikio lakini furaha yake itatimia akilinasa penzi la Diamond ambalo linawindwa na wasichana wengi.
Ray C alipotafutwa ili kutolea ufafanuzi madai hayo simu yake ilikuwa busy muda wote.
Kwa upande mwingine Diamond alipotafutwa na kupatikana alisema:
"Kaka mimi sina taarifa kabisa na habari hizo, kwangu Ray C namchukulia kama dada yangu"
0 comments:
Post a Comment