SIKU chache baada ya msanii anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya
filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kuingia kwenye kumi
na nane za mtego wa kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu
‘OFM’, ameibuka na kusema, anajuta, amekoma na hatarudia tena.
Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika ofisi za GPL akiongea na OFM.
Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa kujiuza iliripotiwa na gazeti
damu moja na hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita, ambapo msanii huyo
aliingia mkenge baada ya kukubali kukutana na ‘pedeshee’ mmoja kutoka
mkoani kwa lengo la kumpa uroda kwa malipo ya shilingi 500,000.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, Jumatatu jijini Dar es
Salaam, Vai alisema: “Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini
pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba ndugu zangu na mashabiki wangu
wote wanisamehe kwa dhati kabisa.
“Naahidi sitarudia tena ujinga kama ule. Ilikuwa ni tamaa tu. Hivi
ninavyozungumza na wewe nipo kwa editor (mhariri) nasimamia editing
(uhariri) ya filamu yangu ambayo ipo katika hatua za mwisho kuingia
mitaani. Niko bize na kazi, acha niwekeze kwenye ujasiriamali tu.
Nawashauri wasanii wenzangu tutulie maana OFM wapo macho.”
Alisema, katika filamu yake hiyo aliyoipa jina la Beautiful Liar
amewashirikisha wakongwe Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Hashim Kambi
‘Wingo’ na mastaa wengine kwenye tasnia hiyo na kwamba mashabiki wake
wakae mkao wa kula.
Kuomba msamaha ni uungwana, ikiwa Vai umeona kosa lako na kuomba radhi ni jambo zuri la kupongezwa. Tunakutakia kila la heri katika mabadiliko hayo, tukikusisitiza iwe kweli maana OFM bado ipo kazini. – MHARIRI.
0 comments:
Post a Comment