Wednesday, February 5, 2014


Tatizo hili limekuwa kama la kawaida majumbani mwetu ila lina madhara makubwa kama likikupata.

Tukio hili la kuumiza limetokea hivi karibuni.

Mke alikuwa jikoni akijiandaa kupika na kwa bahati mbaya akaungua na moto wa gesi na mme bado amelazwa kwa muda mrefu sasa akiuguza majeraha makali yaliyosababishwa na moto wakati akimwokoa mkewe.

Jinsi ilivyotokea:

Jiko la gesi liliwashwa kwa ajili ya kupika na mama huyu wakati huku akiwa hajaweka kitu akaona mende wengi karibu na jiko na kuchukua dawa ya kuua wadudu na kuwapulizia mende waliokuwa karibu na jiko la gesi ambalo lilikuwa linawaka.

Kukatokea mlipuko mkubwa kwa kuwa dawa ile pia ni gesi na mama nguo zake zikadaka moto na kuanza kuungua.

Mme akaja haraka akijitahidi kuuzima moto na kumtoa mkewe kwenye moto lakini moto ulishapamba na kuwa mkubwa na mtungi wa gesi hatimaye kubasuka na kuongezeka kuwa mkubwa.

Wakafanikiwa kutolewa na majirani na kukimbizwa hospitali ambako mme bado yuko kwenye wodi ya watu mahututi na hajui kama mke alikufa kabla ya kufika hospitali.

Hebu nasi tuelewe haya:

Dawa za kuulia wadudu zile tunazo-spray ni mbaya kwenye moto kwani hulipuka kama gesi nyingine.

Dawa ya kupuliza husambaa mapema na kujichanganya na oxygen jambo ambalo ni hatari kwa afya yako

Tafadhali Comment R.I.P kwa mama huyu aliyefariki na share ujumbe huu kuifundisha na kuitahadharisha familia yako na marafiki unaowajali ili kuokoa maisha yako nawe utabarikia


Credit: .tabasamunafuledi

0 comments:

Post a Comment

Click here

Click here

Popular Posts