Watu wawili
wamekamtwa kwa tuhuma za mauaji ya Sista Clesencia Kapuli (50) wa Kanisa
Katoliki, aliyekuwa Mhasibu katika Shule ya Sekondari Mwenyeheri,
jijini Dar es Salaam.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema watu hao ni kati ya
watu wanane waliokamatwa kwa tuhuma za ujambazi sugu wa kutumia silaha.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alisema watu hao
walikamtwa juzi katika operesheni iliyofanywa na jeshi hilo kwa kutumia
vikosi maalum.
Alisema
licha ya majambazi hao wawili kuhusika katika tukio la mauaji ya sista
huyo, lakini pia walihusika katika tukio la kupora fedha katika benki ya
Barclays tawi la Kinondoni miezi michache iliyopita.
Aliwataja
waliohusika hao wa mauaji ya Mtawa kuwa ni Manase Ogenyeka (35), mkazi
wa Tabata na Hamis Ismail, mfanyabisahara na mkazi wa Magomeni
Mwembechai.
Watuhumiwa
wengine ni Beda Mallya (37), mkazi wa Mbezi Msakuzi; Michael Mushi
(50), mfanyabiashara na mkazi wa Mbezi Makabe; Sadick Mohamed (32),
mfanyabiashara, mkazi wa Mbagala Kizuani; Elibariki Makumba (30); Nurdin
Suleiman (40), wote wakazi wa Buguruni Madenge, pamoja na Mrumis Saleh
(38), mkazi wa Kigogo Freshi.
Pia
Jeshi la Polisi limesema linaendelea na operesheni hiyo pamoja na
kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio la maujai ya
sista Kapuli, Juni 23, mwaka huu, pamoja na jambazi mmoja aliyehusika
katika tukio la wizi wa fedha katika benki ya Barclays.
Sista
huyo ambaye alikuwa mhasibu wa Shule ya Sekondari Mwenyeheri iliyopo
Makoka wilayani Kinondoni, aliuawa Juni 23, mwaka huu kwa kupigwa
risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazio waliokuwa katika
pikipiki aina ya Boxer.
Sista
Kapuli alivamiwa na majambazi hao baada ya kutoka benki Mlimani City
akiwa katika gari aina ya Pick up double cabin yenye namba za usajili T
213 CTZ.
via>>Nipashe
0 comments:
Post a Comment