Mvua
zinaendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi bado zinaonekana
kusumbua kwa baadhi ya maeneo hasa yaliyo mabondeni na sehemu ambazo
mitaro yake ya maji haisafirishi maji vizuri,hii ni mchana wa leo baada
ya mvua hiyo kunyesha ambayo imesababisha usumbufu mkubwa baada ya
maeneo mengi kukumbwa na tatizo la maji mengi ambayo yaliziba barabara
,nyumba za watu pamoja na maeneo mbalimbali.
Mvua hizo ambazo mamlaka ya hali ya hewa pia wametahadhalisha kwamba
zitakuwepo kuanzia Tarehe 5.03.2014 hadi Tarehe 7.03.2014 ,miongoni mwa
sehemu zilizopata usumbufu mkubwa wa mvua hizi ni Hospitali ya
Halmashauri ya Kinondoni Sinza – Palestina baada ya kujaa maji kila kona
na kufanya wauguzi kuacha kazi na kupanda juu ya Meza na viti wakikwepa
maji hayo huku wengine kukimbia katika eneo hilo kuhofia maji hayo.
Sababu kubwa ya kukwepa maji hayo ni kile kinachosemekana kuwa maji
hayo si ya mvua tuu lakini yanakuwa Machafu yaliyochanganyikana na maji
kutoka vyooni ambapo kuna chemba moja ya maji machafu imepita hapo na
baada ya mvua hiyo kwisha inasemekana iliwachukua zaidi ya dakika 30
kufanya usafi kutoa matope yaliyokuwa yamejaa vyumbani.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo amekili kwamba kuhusu usumbufu mkubwa
wa chemba hiyo na mvua hasa katika kipindi hicho ambapo zinanyesha kwa
kiasi kikubwa na kuongeza kuwa kunajuhudi zinahitajika kufanyika ili
kuweza kunusuru tatizo hilo lisiendelee.
Hizi ni baadhi ya picha hizo.
Source:Dar es salaam yetu.
0 comments:
Post a Comment