Katika
hali ya kushangaza wenyeji timu ya Al Ahly mpaka sasa wameshindwa
kuwadhibitishia viongozi wa Young Africans pamoja na Ubalozi wa Tanzania
nchini Misri juu ya Uwanja utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa
marudiano Klabu Bingwa Barani Afrika siku ya jumapili.
Sheria
za mashindano ya CAF zipo wazi na zinaelekeza timu mwenyeji wanapaswa
kuwajulisha wageni uwanja utakaotumika kwa mchezo takribani siku 10
kabla ya mchezo, huku mpaka leo siku ya jumatano takribani siku nne
kabla ya mchezo wakishindwa kutabanaisha mchezo utakapofanyika.Mapema
jana mchana Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Misri Bw Idrisa Juma
alifika makao makuu ya Al Ahly kuweza kujua taratibu za mchezo huo
lakini hakufanikiwa kupata majibu kamili zaidi ya kuahidiwa kufikia leo
mchana kwamba watakua wameshapata majibu juu ya ni sehemu gani mchezo
utafanyika.Afisa
Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto leo asubuhi aliambatana na
maofisa Ubalozi mpaka makao makuu ya klabu ya Al Ahly na kukutana na
meneja Said Abdoulaziz na meneja usalama Morgan na katika mazungumzo
hayo walisema mpaka muda huo walikuwa hawajapata maamuzi ya serikali juu
ya uwanja utakaotumika kwa mchezo.
"Tumeomba
mchezo ufanyike kati ya Uwanja wa Cairo au mji wa Alexandria lakini
Serikali imekataa kutoa Viwanja yake pamoja na ulinzi katika mchezo wetu
kutokana na washabiki wetu kufanya vurugu kwenye mchezo wa Super Cup
dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia" alisema Said.
Katika
kikao hicho kilichofanyika kwa zaidi ya masaa mawili Uongozi wa Young
Africans uliomba mchezo wake ufanyike jijini Cairo kwani ndo sehemu
waliyojiandaa kwa mchezo kufuatia taarifa ya Al Ahly walipokuja Tanzania
kwenye mchezo wa awali.
Mara
baada ya mazungumzo hayo waliahidi kuongea na waziri mwenye dhamana ya
michezo kuruhusu mchezo ufanyike jijini Cairo na kwamba mchezo huo kama
iliyoamuriwa tangu awali na mamlaka husika ya ulinzi na usalama hautakua
na washabiki wowote kwa uwanja wowote utakaochezewa.
Akiongea
na mtandano rasmi wa klabu ya Young Africans Kizuguto amesema wamekaa
kusubiria majibu ya Uwanja utakaotumika kwa mchezo zaidi ya masaa 6 bila
majibu huku viongozi hao wa Al Ahly wakipigiwa simu na kutopokea.
"Tuliwaambia
jiji la Cairol lina Viwanja zaidi ya 10 vyote vyenye hadhi ya kimataifa
sio lazima tucheze Cairo International, wajaribu kuomba viwanja vingine
lakini walionekana kutokua tayari na zaidi kusisitiza watamuomba waziri
wa michezo aruhusu mchezo ufanyike Cairo bila washabiki" alisema
Kizuguto
Kutokana
na mazingira hayo ya ucheleweshwaji kutangaza sehemu utakaofanyika
mchezo Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kupitia Balozi wake Bw Mohamed
Hamza na maafisa wake na uongozi wa Young Africans umeendelea kufanya
maandalizi kwa njia zote kuhakikisha timu inafika salama na kupata
huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na malazi, chakula, uwanja wa mazoezi
na ulinzi kwa kipindi chote timu itakapokuwa nchini Misri.
Msafara
wa watu 30 unatarajiwa kuwasili kesho alfajiri jijini Cairo kwa shirika
la Ndege la Egypt Air na kupokelewa Uwanja wa Ndege na Balozi Hamza,
pamoja na maafisa Ubalozi kisha kuelekea sehemu maalumu ambayo timu
ndipo itakapokua imeweka kambi mpaka siku ya mchezo.
CHANZO : youngafricans
0 comments:
Post a Comment