Mtoto Said Siraji akiwa amelazwa katika Hospital ya wilaya ya Kahama |
Mtukio ya
kikatili yameendelea kushika kasi wilayani Kahama mkoani Shinyanga
ambapo mtoto aitwaye Said Siraji/Said Joshua amelazwa katika Hospitali
ya wilaya usiku wa kuamkia leo, baada ya kunusurika kifo katika jaribio
la kuchinjwa na baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Salvatory.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya-Kahama; Dakta Joseph Fwoma amesema
Siraji amefikishwa hospitalini hapo leo alfajiri baada ya kuokotwa na
wasamaria wema akiwa anakimbia huko akivuja damu shingoni.
Dakta
Fwoma amesema baada ya kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia
upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo aliyochinjwa na hadi alasiri hii
hali yake imeendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa Mariamu Idd(35) amesema, Mtoto Siraji
jana alichukuliwa na baba yake mzazi anayeitwa Siraji Salvatory(45)
kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa wazazi hao walikwisha achana
siku nyingi.
Mariam amesema, awali Salvatory alikuwa akimchukua Siraji mara kwa
mara na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye kumrudisha akidai kuchoshwa
na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya
kiafya.
Jeshi la
polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema
chanzo cha tukio hilo inasadikiwa kuwa mtuhumiwa anaugua ugonjwa wa
akili.
0 comments:
Post a Comment