SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa, msanii wa Bongo Fleva, Astelinah
Sanga ‘Linah’ amenasa ujauzito wa mdosi aitwaye Nagar, ujauzito huo umechoropoka.
Kwa mujibu wa chanzo, ujauzito huo umechoropoka hivi karibuni na
kumfanya Linah kukosa raha kwa kuwa ndoto yake ilikuwa kupata mtoto.
“Ni kweli Linah alikuwa na ujauzito lakini umetoka na amesikitika
sana kwani mdosi wake ni mtu mwenye fedha nyingi na yeye alitamani sana
kuwa na mtoto,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya Linah kutafutwa kupitia simu yake ya kiganjani ili
kupata ukweli wa kutoka kwa ujauzito huo lakini baada ya mwindishi wetu
kujitambulisha, staa huyo alikata simu.
Wiki iliyopita zilizagaa habari za staa huyo kunasa ujauzito wa
mdosi huyo na alipoulizwa alisema habari hizo zilikuwa ni uzushi.
“Nani kakwambia kwamba nina mimba? Hayo ni maneno ya watu,
wanasambaza mitaani sijui hata wameyatoa wapi lakini miye sina mimba,”
alisema Linah na kunukuliwa na gazeti hilo ambalo hutoka mtaani kila
siku ya Jumatano likiwa na habari motomoto za masupastaa.
0 comments:
Post a Comment